Get New DJ Mixes
Blog

ONYANGO AKUBALI KUSEPA SIMBA SC

 

BEKI kisiki wa Simba, Joash Onyango huenda asionekane tena msimu ujao wa Ligi Kuu Bara baada ya kuuomba uongozi wa timu hiyo kuvunja mkataba wake uliobaki ili aende kujaribu maisha mengine ya soka nje ya Simba.

INAYOHUSIANA : KIPA SIMBA SC ABEBA MAMILIONI

Beki huyo alitua nchini Agosti 14, 2020 akitokea Gor Mahia ya nchini Kenya akisaini mkataba wa miaka miwili, aliutumikia kwa mafanikio makubwa na baadaye kuongezwa mwaka mmoja unaotarajia kumalizika msimu ujao.

Habari kutoka ndani ya Simba zilieleza kuwa mchezaji huyo kutokana na lawama za mara kwa mara anazopewa kila anapofanya makosa uwanjani ameomba kumalizana nao ili aondoke.