Get New DJ Mixes
Blog

KIPA SIMBA SC ABEBA MAMILIONI

 

Ally Salim amekabidhiwa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month) mwezi Aprili, 2023.

Kipa huyo amekuwa chaguo la kwanza ndani ya kikosi cha Simba kwenye mechi za hivi karibuni baada ya kipa namba moja Aishi Manula kupata maumivu.

Salim alikaa langoni kwenye mchezo dhidi ya Yanga uliokamilika kwa ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Simba 2-0 Yanga.

Mchezo wake wa kwanza ilikuwa dhidi ya Ihefu ambapo ubao wa Uwanja wa Highland Estate pale Mbeya Ulisoma Ihefu 0-2 Simba.

Mchezo ambao Manula alipata maumivu ilikuwa dhidi ya Ihefu ambao ulikuwa ni wa Kombe la Shirikisho hatua ya robo fainali ubao wa Uwanja wa Azam Complex uliposoma Simba 5-1 Ihefu.

Kwenye mechi ya hatua ya nusu fainali ya Azam Sports Federation Salim alikaa langoni na ubao wa Uwanja wa Nangwanda Sijaona ukasaoma Azam FC 2-1 Simba hiyo ilikuwa ni Mei.

Kipa huyo alikuwa anapambana na Jean Baleke pamoja na Kibu Dennis ambao aliingia nao fainali yeye kuibuka mshindi na kusepa na mkwanja wa milioni mbili.