
Taarifa zinazozidi kusambaa zinaeleza kuwa mtangazaji maarufu wa kipindi cha Lavi Davi, Diva The Bawse, huenda ameagana rasmi na Wasafi FM baada ya kumaliza mkataba mpya na kituo hicho.
Kwa muda mrefu sasa, Diva hajaonekana hewani, jambo lililowafanya mashabiki wengi kuhoji alipo. Akijibu mmoja wa mashabiki kupitia mtandao wa kijamii, Diva alidai kuwa ameamua kutoongeza mkataba mpya baada ya ule wa awali kumalizika.
Hadi sasa bado hakuna taarifa rasmi kuhusu hatua yake inayofuata, hivyo mashabiki wanasubiri kujua ataelekea wapi baada ya kuondoka Wasafi FM.
Endelea kufuatilia IK MZIKI kwa taarifa zaidi kuhusu sakata hili na habari nyingine za burudani.
#DivaTheBawse #WasafiFM #LaviDavi #IKMziki #Burudani #TanzaniaEntertainment
