
Msanii na muigizaji wa filamu Cholo Kobisi amefunguka kuhusu maisha yake ya mapenzi akisema kuwa kwa sasa yupo kwenye mahusiano, lakini hana mpenzi rasmi kwa sababu bado hajampata mtu sahihi wa kuwa naye.
Akizungumza kuhusu hilo, Cholo Kobisi amesema, “Yeah nipo kwenye mahusiano, yani nina mahusiano lakini sina mpenzi. Yani sina mtu ambaye hana kipingamizi ambaye huyu ni wa kwangu.”
Kauli yake imeibua mjadala miongoni mwa mashabiki wake, wengi wakitaka kufahamu zaidi kuhusu hali yake ya sasa kimapenzi. Endelea kufuatilia IK MZIKI kwa habari zaidi za burudani na mastaa mbalimbali.
#CholoKobisi #Burudani #Mahusiano #IKMziki #CelebUpdates
