
Mwijaku amemkosoa vikali Diamond Platnumz akidai kuwa amechangia kuuharibu muziki wa Tanzania kutokana na kile alichokiita majivuno na kuamini kuwa tayari ameshafika.
Kauli hiyo imekuja muda mfupi baada ya Meneja Mkuu wa Digital wa WCB, Kim Kayndo, kusema kuwa baadhi ya media na waandishi wa habari hawaupendi muziki wa Tanzania.
Akizungumza kuhusu hilo, Mwijaku amesema, “Kaa tafakari msanii wako alikosea nini, alipunguza nini, kwa sababu msanii wako alijiona amefika, kwa hiyo cha kwanza lazima aondoe majivuno.”
Kauli hizi zimezua mjadala mkubwa mitandaoni huku mashabiki wakitoa maoni yao tofauti kuhusu suala hilo. Endelea kufuatilia IK MZIKI kwa updates zaidi za burudani na muziki.
#Mwijaku #DiamondPlatnumz #WCB #IKMziki #BongoFlava #Burudani
