E NEWS

MBIWDO MC AACHANA NA WABONGO, AJIUNGA RASMI NA LEBO YA WATOTO WA USWAHILI

Download | Play Now
MBIWDO MC AACHANA NA WABONGO, AJIUNGA RASMI NA LEBO YA WATOTO WA USWAHILI

Msanii wa Singeli anayefanya vizuri na maarufu kwa jina la Mbiwdo MC ameandika ukurasa mpya katika safari yake ya muziki baada ya kuachana rasmi na lebo ya Wabongo na kujiunga na lebo ya Watoto wa Uswahili.

Kwa kipindi kirefu, Mbiwdo MC alifahamika akiwa chini ya lebo ya Wabongo, inayomilikiwa na wakali wawili Chief Killer na Babilon Samas, ambapo alijijengea jina na mashabiki wengi kupitia kazi zake za Singeli.

Hatua hii ya Mbiwdo MC kuondoka Wabongo inakuja muda mfupi baada ya mmoja wa wamiliki wa lebo hiyo, Chief Killer, kutangaza wazi kwa umma kuwa kwa sasa lebo ya Wabongo imebaki na wasanii wawili tu, yaani Chief Killer mwenyewe na Babilon Samas.
Chief Killer alithibitisha taarifa hiyo moja kwa moja kwa IK MZIKI kupitia mawasiliano ya chat, jambo linaloonyesha mabadiliko makubwa ndani ya lebo hiyo.

Kwa kujiunga na Watoto wa Uswahili, Mbiwdo MC anatarajiwa kufanya kazi kwa karibu na Msaka Daily, mwanzilishi wa lebo hiyo, ambaye amekuwa mstari wa mbele kukuza na kusukuma muziki wa Singeli unaotoka moja kwa moja mitaani.

Mashabiki wengi sasa wanatazamia kuona mwelekeo mpya wa muziki wa Mbiwdo MC, ubunifu zaidi na kazi kali zitakazotoka chini ya lebo yake mpya.

Endelea kufuatilia IK MZIKI kwa taarifa zaidi, nyimbo mpya na habari zote moto kutoka kwenye tasnia ya Singeli Tanzania.

#MbiwdoMC #WatotoWaUswahili #Wabongo #Singeli #IKMZIKI