
Mwaka 2010, kata ya Kaloleni ilimchagua RASTAMAN aitwaye Mpanda kuwa diwani kwa tiketi ya CHADEMA, na hakuwahi kushinikizwa kunyoa dread zake.
Mwaka 2015 kulikuwa na kipenzi chetu, dada yetu Magreth Samson David. Alikuwa na dread pia, na hakuna aliyemwambia azinyowe.
Wote hao walikuwa madiwani wa Jiji la Arusha, ambako nami nilihudumu. Walikuwa salama jinsi walivyo, kwa kuwa walikuwa pia waongoza utalii, kazi ambayo kuwa na rasta ni jambo la kawaida kabisa.
Nyimbo ya Mwisho ya Dogo Janja : Dogo Janja Ft. Aslay – One Day
Leo tuna Ngarenaro Finest – @dogojanjatz
Mwanamuziki mahiri.
Icon tangu akiwa mdogo.
Waliomlea wameamua awe kiongozi. Wamemchagua alivyo.
Lakini wenye roho mbaya wameanza kuhoji kuwa anawezaje kuwa diwani na bado akawa na rasta. Wamesahau waliopita katika halmashauri hii hii, ambao hawakuwahi kubughudhiwa.
Janjaro ni mwanangu.
Nitasimama naye kwenye hili.
Aachwe ahudumie waliomuamini, maana daima amejivunia na kuitangaza ardhi aliyozaliwa—Ngarenaro.
@madeeali ulipomlea, Ngarenaro ilikupa heshima ya kuchagua.
Aachwe afanye kazi.
Heshima kwa Rasta!
