E NEWS

DULLAH MAKABILA : HAINA JINSI INABIDI KILA KITU TUMUIGE MBOSSO

DULLAH MAKABILA HAINA JINSI INABIDI KILA KITU TUMUIGE MBOSSO

Mfalme wa Singeli, Dullah Makabila, amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu ubunifu wa msanii mkubwa wa Bongo Fleva Mbosso. Kupitia comment section ya mitandao ya kijamii, Dullah alikiri wazi kuwa kwa sasa kila kitu cha ubunifu kinachoonekana kwenye muziki kinamfanya kumuiga Mbosso, kwani hana namna nyingine.

Nyimbo ya Dullah Makabila Mpya : Dulla Makabila Ft. Mack Zube – Makolo

Kauli hiyo ilikuja baada ya shabiki aliyejitambulisha kama Hanscana kusema kuwa kile ambacho Dullah anajaribu kufanya tayari Mbosso alishafanya miaka kumi iliyopita. Badala ya kupuuzia, Dullah Makabila alijibu moja kwa moja na kukubali kuwa ni kweli kwa sasa Mbosso ndiye msanii anayebeba bendera ya ubunifu, na wasanii wengine wanajifunza kupitia kwake.