E NEWS

Dogo Paten Kurudi kwa Kishindo Leo na Ngoma Mpya Inayoitwa Je Ungeweza

Dogo Paten Kurudi kwa Kishindo Leo na Ngoma Mpya Inayoitwa Je Ungeweza

Msanii anayechipukia kwa kasi kwenye Singeli, Dogo Paten, ambaye aliwahi kutamba na ngoma kali “Afande” aliyomshirikisha staa wa WCB Zuchu, anarudi tena kwa kishindo!

Baada ya ukimya wa muda mfupi, leo hii Dogo Paten ametangaza rasmi kuwa atatoa wimbo mpya unaoitwa “Ungeweza”. Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, msanii huyo amewaambia mashabiki wake kuwa muda umefika wa kuachia kazi ambayo inatoka moyoni.

Track Yenyewe Hii hapa : Dogo Paten – Ungewezaje

Hii ni ngoma ambayo mashabiki wengi wamekuwa wakingojea kwa hamu kubwa, wakitaka kuona kama atarudi na nguvu ileile aliyokuja nayo kupitia Afande, kazi iliyotikisa redio na mitaa kote Tanzania.

“Ungeweza” inatarajiwa kutoka leo saa kamili. Jiandae kuisikiliza kwenye platforms zote maarufu.

Ujumbe wa Dogo Paten kwa Mashabiki:

“Ni muda wa kutoa kilichonisumbua moyo… ‘Ungeweza’ drops today.” – Dogo Paten kupitia Instagram

Je, una matarajio gani na wimbo huu mpya wa Dogo Paten – “Ungeweza”?
Unadhani ataweza kurudia mafanikio ya Afande au hata kuyazidi?

Endelea kutufuatilia hapa IK MZIKI kwa updates zote za ujio huu, video rasmi, na maoni kutoka kwa mashabiki!