Msanii wa Singeli Kidene Fighter ametuma ujumbe mzito kwa wasanii wenzake kupitia Instagram. Kupitia ukurasa wake, ameandika:
“Wasanii wa Singeli toeni nyimbo zenu mapema kabla sijaachia album yangu… msije kusema sikusema!”
Kidene ametangaza ujio wa album yake mpya iitwayo KUMI ZA MOTO, ambayo itakuwa na nyimbo kumi pekee. Anasema album hii italeta mageuzi makubwa kwenye muziki wa Singeli, huku akiweka wazi kuwa itarudisha ladha ya Kidene wa zamani pamoja na ubunifu wa Kidene wa kisasa. Kwa maneno yake mwenyewe:
“Mashabiki zangu najua mnahitaji kunisikia… basi album hii itakata kiu yenu yote.”
Amesema pia mitaa itaenda kwa jina la CHIMWALI PAULO WW, na akasisitiza mashabiki wake waendelee kumpa sapoti huku akimalizia na:
“MSICHOKE KUNISAPOTI – MUNGU AWABARIKI WOTE!”