E NEWS KAZALIWA

LEO TAR 3 MWEZI WA 6 KAZALIWA CURTIS MAYFIELD – NGULI WA SOUL & RNB

Download | Play Now
LEO KAZALIWA CURTIS MAYFIELD - NGULI WA SOUL & RNB

Leo tarehe 03 Juni, dunia ya muziki inamkumbuka nguli wa Soul na R&B, Curtis Mayfield, ambaye alizaliwa siku kama ya leo mwaka 1942 katika jiji la Chicago, nchini United States.

Curtis Mayfield alikuwa mwimbaji, mtunzi wa nyimbo, mpiga gitaa na mtayarishaji wa muziki aliyefanikiwa kuacha alama kubwa katika historia ya muziki duniani. Alitamba kupitia muziki wa Soul, R&B na Funk, huku akitambulika kwa nyimbo zenye ujumbe mzito wa kijamii na maisha ya kila siku.

Nguli huyo anatajwa kuwa mmoja wa wasanii waliochangia kwa kiwango kikubwa maendeleo ya muziki wa kisasa na amekuwa chanzo cha msukumo kwa wasanii wengi duniani.

Licha ya kufariki dunia mwaka 1999, kazi zake bado zinaendelea kusikilizwa na kuheshimiwa na mashabiki wa muziki katika mataifa mbalimbali.

IK MZIKI tunamtakia kumbukumbu njema nyota huyu wa muziki ambaye alichagua tarehe ya leo kuja duniani na kuandika historia yake katika tasnia ya burudani.

Endelea kutufuatilia IKMZIKI.COM kwa habari za muziki, Singeli, Bongo Fleva na burudani kutoka Tanzania hadi duniani kote.

#CurtisMayfield #WaliozaliwaLeo #IKMziki #June3 #MusicHistory #SoulMusic #RNB #EntertainmentNews #BongoFleva #Singeli #IKMZIKI