
Mashabiki wa Singeli jiandaeni kwa ujio mpya wenye kishindo kutoka Mbanje Choba MC. Msanii huyu maarufu wa Singeli ametangaza kurejea rasmi kwenye ramani ya muziki baada ya kimya cha muda mrefu, safari hii akija na EP mpya inayotarajiwa kutikisa mtaa.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka IK MZIKI, EP hiyo itakwenda kwa jina la Maumivu, mradi unaobeba vibao vizito, hisia halisi na simulizi za kweli za maisha ya mtaa. Choba MC anarudi na nguvu mpya, ubunifu wa tofauti na ladha ya Singeli inayogusa mashabiki wa kweli.
Huu ni mwanzo mpya kwa Choba MC na mashabiki wake, hivyo kaa tayari kwa makubwa zaidi. Endelea kutufuatilia kupitia mitandao yetu ya kijamii ya IK MZIKI kwa updates zote za uhakika kuhusu EP hii na habari nyingine za muziki.
#IKMziki #ChobaMC #MaumivuEP #Singeli #SingeliMusic #MbanjeFinest #UjioMpya #MuzikiWaMtaa
