E NEWS SINGELI

LEO KAZALIWA MSANII WA SINGELI MAARUFU KAMA PALU SIMELA

Download | Play Now
LEO KAZALIWA MSANII WA SINGELI MAARUFU KAMA PALU SIMELA

Leo tarehe 25 Desemba, kazaliwa msanii wa muziki wa Singeli maarufu kama Palu Simela, kutoka Temeke, Dar es Salaam – Tanzania.Palu Simela ni msanii wa Singeli wa muda mrefu ambaye amedumu kwenye tasnia kwa miaka mingi, akijizolea mashabiki wengi kupitia muziki wake wenye kasi, ujumbe wa mtaani na vionjo halisi vya Singeli ya Temeke.

Katika safari yake ya muziki, Palu Simela amefanikiwa kufanya vibao vikubwa na kushirikiana na wasanii mbalimbali wakubwa wa Singeli na Bongo Fleva, akiwemo: Amber Lulu,Mudy Msanii,Balaa MC,MC NK
na wengine kadhaa.

Kupitia kazi zake, Palu Simela ameendelea kuutangaza muziki wa Singeli ndani na nje ya Tanzania, na kubaki kuwa miongoni mwa wasanii wanaoheshimika katika mtaa wa Singeli.IK MZIKI inaendelea kuweka kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwa wasanii na wadau wa burudani kutoka Tanzania, Afrika na dunia nzima.

#IKMZIKI #KazaliwaLeo #PaluSimela #Singeli #Temeke #DarEsSalaam #BurudaniTanzania #SingeliOriginal