E NEWS

DJ MUSHIZO : NILIKATA TAMAA YA MAISHA KAMA NINGEWEZA KUISHI TENA

DJ MUSHIZO NILIKATA TAMAA YA MAISHA KAMA NINGEWEZA KUISHI TENA

Baada ya ukimya wa muda mrefu, DJ maarufu wa Singeli DJ Mushizo hatimaye amevunja ukimya kupitia ukurasa wake wa Instagram. Ameandika ujumbe wenye kugusa moyo, akieleza jinsi safari yake ya kupona baada ya ajali ya moto ilivyokuwa ngumu lakini ikamfundisha thamani ya matumaini, imani na upendo wa karibu zake.

NYimbo ya Mwisho ya DJ Mushizo : Dj Mushizo Ft. Jetty Mc & Vanillah – Mapenzi Hisia  | Download

“Kila jeraha lina hadithi yake, na yangu ni ya mapambano na matumaini. Safari ya uponyaji haikuwa rahisi, kulikuwa na siku nilihisi kukata tamaa, lakini upendo, imani kwa Mungu na msaada wa watu wangu ulinipa nguvu mpya. Mungu amejibu maombi yetu,” aliandika DJ Mushizo.

Kupitia ujumbe huo, amewashukuru wote waliomuombea na kusimama nae kipindi kigumu. Sasa ameahidi kuanza ukurasa mpya wa maisha na kazi yake ya muziki.

Endelea kufuatilia taarifa na updates zake kupitia mitandao ya kijamii ya @ikmziki.