E NEWS

Zuchu Kuwasha Moto Jukwaa la Afcon Kenya 2025

Zuchu Kuwasha Moto Jukwaa la Afcon

Mashabiki wa soka na burudani wanatarajia sherehe kubwa Jumamosi hii, pale Uwanja wa Kasarani, Nairobi, ambapo fainali ya michuano ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) itapigwa kati ya Madagascar na Morocco. Mbali na mvuto wa soka, upande wa burudani pia umepangwa kuwasha moto baada ya kuthibitishwa kwamba Zuchu, nyota wa Bongo Fleva, atashiriki kwenye onyesho hilo akipanda jukwaa pamoja na Eddy Kenzo wa Uganda na Savara kutoka kundi la Sauti Sol.

Sikiliza Nyimbo ya Zuchu hapa : Zuchu – Amanda

Hii itakuwa mara ya pili kwa msanii wa Tanzania kushiriki kwenye jukwaa la CHAN mwaka huu, kwani Rayvanny ndiye aliyepewa nafasi ya kufungua michuano hiyo mapema Agosti 2 katika Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zuchu hakuficha furaha yake, akieleza wazi kuwa anahisi heshima kubwa kuwakilisha Tanzania kama msanii mkuu katika fainali hiyo.

Kwa Tanzania, hii ni hatua ya kujivunia, si kwa sababu pekee ya kuwa moja ya waandaaji wa mashindano, bali pia kwa kutambua mchango mkubwa wa wasanii wake katika tasnia ya muziki barani Afrika.

Mashindano ya mwaka huu yamekuwa ya kipekee kwani yalihusisha nchi tatu za Afrika Mashariki – Kenya, Uganda na Tanzania – ambazo zote ziliingia robo fainali. Hata hivyo safari zao zilikatika mapema: Tanzania ilibanduliwa na Morocco kwa bao 1-0, Kenya ikaaga kupitia mikwaju ya penalti dhidi ya Madagascar, na Uganda ikaondoshwa na bingwa mtetezi Senegal.

Also,more tracks from Zuchu:

AUDIO : Zuchu – Oktoba Tunatiki
AUDIO : Zuchu Ft. Lava Lava – Cherie
AUDIO | Zuchu Ft. D Voice – Hujanizidi | Download
ALBUM | Zuchu – Peace and Money (13 Track Hit Song)