Mdundo Yaendeleza Dhamira Yake kwa Wasanii wa Tanzania kwa Msaada Mkubwa wa Vodacom Tanzania PLC katika Malipo ya Mirabaha 2025
Mdundo, jukwaa kinara barani Afrika la usambazaji wa muziki, linaendelea kubadilisha tasnia ya muziki kwa kuwawezesha wasanii kusambaza, kutangaza na kupata kipato kupitia kazi zao. Kwa idadi ya watumiaji inayozidi milioni 38.7 kwa mwezi na shughuli katika nchi mbalimbali za Afrika, Mdundo linaendelea kuwa mstari wa mbele katika mapinduzi ya kidijitali ya muziki barani Afrika.
Mwezi Januari 2025, Mdundo lilianza msimu wake wa malipo ya mirabaha ya kila nusu mwaka, ambayo yanaendelea kwa sasa, na yananufaisha zaidi ya wamiliki wa haki zaidi ya 100,000 barani kote, wakiwemo maelfu ya wasanii wa Kitanzania. Tangu kuanzishwa kwake, jukwaa hili limewalipa wasanii zaidi ya 200,000, huku idadi ya wanufaika ikiongezeka kila msimu wa malipo. Hii ni hatua kubwa inayoonyesha dhamira ya Mdundo ya kujenga ekosistemi endelevu ya muziki kwa wasanii wa Kiafrika hasa wasanii wa Kitanzania.
Martin Nielsen, Mkurugenzi Mtendaji wa Mdundo, alieleza kwa fahari mafanikio ya jukwaa:
“Dhamira yetu siku zote imekuwa kuwapa wasanii wa Kiafrika jukwaa endelevu la kustawi. Kwa kutoa mapato ya uhakika na yenye tija, tunachangia katika kukuza wasanii binafsi huku tukisaidia maendeleo ya muda mrefu ya tasnia ya muziki barani Afrika kwa ujumla.”
Moja ya nguzo muhimu za mafanikio haya nchini Tanzania imekuwa ushirikiano madhubuti kati ya Mdundo na Vodacom Tanzania PLC, kampuni inayoongoza ya mawasiliano nchini. Kupitia ushirikiano wa kifurushi cha usajili na ubunifu wa bidhaa, Mdundo imewezesha upatikanaji rahisi wa muziki kwa mamilioni ya Watanzania. Hatua hii imepanua hadhira kwa wasanii, kuongeza mapato, na kuchangia moja kwa moja malipo ya royalty kwa maelfu ya wamiliki wa haki nchini.
Sowari Akosionu, Afisa Mkuu wa Masoko wa Mdundo, alisisitiza nafasi muhimu ya Vodacom Tanzania PLC: “Ushirikiano wetu na Vodacom Tanzania PLC umekuwa msingi mkubwa wa kuwezesha malipo ya mirabaha nchini. Kupitia mtandao wao mpana, Vodacom inawawezesha wasanii wa ndani kuongeza kipato na kuimarisha ekosistimu ya muziki ya Kitanzania.”
Mbali na hayo, katalogi ya Mdundo inajumuisha muziki wa kimataifa na pia muziki wa Kitanzania kuanzia Bongo Flava hadi Singeli. Mbinu hii ya kulenga muziki wa ndani inaimarisha uhusiano na wasikilizaji wa Kitanzania, inaongeza mwonekano wa wasanii wa kanda, na inaunda vyanzo vipya vya kipato kwa wamiliki wa haki.
Kwa kuangalia mbele, Mdundo inalenga kugawa jumla ya kati ya Dolla za Kimarekani, milioni 2.1 hadi 2.3 kufikia mwaka 2026, huku msisitizo ukiwa juu ya kuinua wasanii wa ndani na kuonyesha vipaji vya Kitanzania kwenye jukwaa la kimataifa.
Kupitia teknolojia rahisi kutumia, mitandao mikubwa, na ushirikiano madhubuti kama huu na Vodacom Tanzania PLC, Mdundo linaendelea kuwapa wasanii wa Kitanzania fursa ya kukuza muziki wao, kupanua hadhira, na kuongeza kipato chao.
Endelea kuenjoy DJ Mixes hapa: https://mdundo.ws/DjNahMixes