Historia ya Dogo Paten – Msanii wa Singeli
Dogo Paten ni msanii wa muda mrefu katika muziki wa Singeli ambaye anatokea Mbezi, Dar es Salaam. Alianza muziki akiwa bado mtoto mdogo, akishiriki katika majukwaa mbalimbali ya kusaka vipaji kama E FM Funga Mtaa, na mingineyo.
Mara ya kwanza alisimamiwa na meneja wake wa zamani anayejulikana kama Badloso, ambaye alimpa sapoti kubwa katika hatua za awali za muziki wake. Baada ya tofauti baina yao, kwa sasa Dogo Paten anajitegemea.
Umaarufu Wake Ulivyoanza – Salio na TikTok
Dogo Paten alivuma sana baada ya video yake kusambaa kwenye TikTok, akilalamika kutengwa na wasanii wenzake baada ya kutoa ngoma kali Salio aliyoshirikiana na Mdogo Sajent. Video hiyo iliwauma mashabiki wengi ambao waliguswa na hali yake, na hivyo kuanza kumpa sapoti kubwa mtandaoni.
Kupitia viral hiyo, alialikwa kwenye mahojiano na vyombo vingi vya habari vikubwa akiwa na meneja wake Badloso. Katika mahojiano hayo, Badloso alifunguka kuhusu hali halisi ya Dogo Paten, akieleza namna alivyomsapoti wakati wenzake wakimtenga.
Zuchu Amuweka Juu – Nyimbo ya “Afande”
Baada ya tukio hilo kugusa hisia za mashabiki wengi, msanii maarufu wa Bongo Fleva Zuchu aliibuka na kuachia wimbo Afande, akimshirikisha Dogo Paten na kumtambulisha rasmi kwa mashabiki wake, huku akiwataka watanzania kumsaidia dogo huyu mwenye kipaji kikubwa.
Tangu hapo, jina la Dogo Paten limekuwa kubwa, akawa maarufu sana, na mpaka sasa ameanza kuachia nyimbo zake binafsi ambazo zinaendelea kufanya vizuri kwenye mitandao ya muziki.
Dogo Paten – Orodha ya Nyimbo Zake Mpya (Audio Download)
Hapa chini ni orodha ya baadhi ya nyimbo kali kutoka kwa Dogo Paten ambazo unaweza kuzisikiliza au kupakua moja kwa moja.
- Dogo Paten Ft. Mdogo Sajent – Salio – Download Audio
- Dogo Paten – Afande Ft. Zuchu – Download Audio
- Dogo Paten – Ungewezaje – Download Audio
- Dogo Paten – Sikupendi (karibia kutoka) – [COMING SOON]
Mahojiano na Dogo Paten (Media Appearances)
Tazama baadhi ya interview ambazo Dogo Paten alifanya na vyombo vikubwa vya habari akieleza maisha yake, changamoto na safari yake ya muziki.
Interview na Wasafi
Exclusive Interview na EATV –
Maelezo ya Badloso kuhusu Dogo Paten –
Wasanii Aliowahi Kufanya Nao Kazi
- Zuchu – Kupitia wimbo wa Afande
- Mdogo Sajent – Kupitia wimbo wa Salio
- Deeluck – Ushirikiano wa ndani ya label