E NEWS AUDIO

CHILILY NOMAN KUIZIMA MITAA NA KWA WAKATI

Msanii wa Singeli anayezidi kupaa kwa kasi kwenye anga la muziki wa mtaani, Chilily Noman, yuko mbioni kutambulisha kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la β€œKwa Wakati” – ngoma kali yenye mashairi yenye mzuka na ujumbe mzito, itakayowasha moto kwenye kila kona ya burudani.

Ngoma hii imefanyika chini ya mikono ya Producer Banny, mmoja wa watayarishaji wanaosifika kwa kuzalisha sauti kali na zenye nguvu ndani ya game ya Singeli. Kazi hii ni uthibitisho kuwa Chilily Noman, kutoka kwenye lebo ya Macode, yuko tayari kuchukua nafasi yake kama mmoja wa vinara wa Singeli ya kisasa.

Kwa Wakati itapatikana rasmi hapa hapa kwenye Ik Mziki, hivyo mashabiki wa Singeli na muziki wa mtaa kwa ujumla, kaeni mkao wa kula!

πŸ”₯ Chilily Noman – Kwa Wakati
🎧 Produced by Banny
🏷️ Macode Label
πŸ“ Exclusively on Ik Mziki

#KwaWakati #ChililyNoman #Singeli2025 #IkMziki #MacodeLabel