Mdundo.com na sanaa ya Kitamaduni Barani Afrika
Umewahi kukutana na wimbo wenye mdundo unaovutia ambao unawakilisha mizuka wa mji wako,lugha yako , kijiji chako, au tamaduni zako? Hiyo basi ndio lengo kuu la mdundo kuamua kufikia tamaduni zako kwa kukupa fursa ya kupakua mziki wa kitamaduni au wa lugha za kiafrika ambazo ni tofauti tofauti. Hivyo katika makala haya ya “Mdundo Story” tunaangazia jinsi ya kuwezesha wasanii wa mziki wa asili yetu ya Kiafrika na jinsi wanaweza kujitengezea kipatao kupitia jukwaa mdundo.com
Filamu hi inaangazia dhamira ya Mdundo ya kuonyesha muziki wenye ladha tofauti ya eneo husika. Inajumuisha mahojiano na watu mbalimbali kutoka katika tasnia ya muziki, kila mmoja akitoa mtazamo wake wa kipekee kuhusu muziki wa kiasili ya lugha za kiafrika. Wanamuziki mashuhuri wanazungumzia umuhimu wa muziki unaoonyesha uzoefu na desturi za jamii ya maeneo mbali mbali. Wasanii chipukizi wanashiriki jinsi majukwaa kama Mdundo yanavyowasaidia kupanua wigo wao ndani ya mkoa wao wenyewe.
Pia tunaonyesha nguvu ya muziki wa kitamaduni ama asilia katika sehemu mbalimbali za Afrika. Kupitia sehemu hizi, makala haya yanasisitiza umuhimu mkubwa wa kitamaduni wa muziki wa Afrika.
Ni muhimu kutazama kwa mtu yeyote anayevutiwa na tasnia ya muziki ya Kiafrika yenye nguvu na uwezo wa yaliyo ya ndani kuunda uhusiano wa kina kati ya wasanii na watazamaji.
Tazama hapa: https://www.youtube.com/watch?v=E8ITt-TS4Ac