Get New DJ Mixes
ENTERTAINMENT MUSIC

Diamond Platnumz Atangaza Kuachana na Zuchu ‘I’m Single Boy’

Katika gumzo la hivi karibuni, staa wa Bongo Flava, Diamond Platnumz, amejitokeza kwenye ukurasa wake wa insta kutangaza kuwa sasa yeye ni ‘single boy.’ Hii inajiri wakati tetesi zikiwa zinazidi kuhusu uhusiano wake na mwenzake kutoka lebo hiyo, Zuchu.

Diamond alisema, “Kuanzia leo ningependa kutangazia rasmi kuwa MIMI NI SINGLE, sipo kwenye uhusiano, wala sina mahusiano na mwanamke yeyote.” Tangazo hili linakuja baada ya mama yake Diamond, Bi. Dangote, kukanusha uvumi kuhusu uhusiano wa kimapenzi kati ya Diamond na Zuchu.

Also, check more tracks from Diamond Platnumz;

 

 

Mambo yalichukua mkondo mwingine baada ya Mange Kimambi, maarufu kama ‘dada wa Taifa,’ kutoa maoni yake. Mange anaonekana kufurahishwa na kuvunjika kwa mahusiano ya Diamond na Zuchu, akidai kuwa Zuchu alikuwa akimroga Diamond ili ampende. Mange anamshauri Diamond asiende tena kwa Zuchu, akisema kuwa Zuchu hawezi kudumisha uhusiano wa kudumu na mtoto wa Mama Dangote.

Mange anaenda mbali kwa kusema atampatia Diamond mwanamke mwenye hadhi, tofauti na Zuchu ambaye anadaiwa kukosa mvuto. Mwishowe, Mange anatoa onyo kwa Diamond kusoma dua ili kuepuka uchawi wa Zuchu na mama yake.

Hii ni mojawapo ya mikasa ya mapenzi inayopata umaarufu katika tasnia ya burudani nchini Tanzania, na mashabiki wanangojea kwa hamu kujua jinsi mambo yatakavyokwenda.